DIWANI
wa kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Keneth Yindi amewataka vijana kutumia fursa
walizokuwanazo za ujana katika kuisaidia serikali kuinua uchumi wake ikiwemo wa
kijamii na kiroho.
Yindi
amesema hayo alipokuwa akizungmza na vijana wa kanisa la Anglikan parishi ya
maili mbili Dodoma kwenye harambe ya kuchangia uziduzi wa albamu.
Amesema
vijana wanayo nafasi kubwa ya kutumia fursa zilizopo katika kuinua uchumi wa
Tanzania na hatimaye kuleta maendeleo,badala ya suala hilo kuachia serikali na wadau
wengineo wakiwemo taasisi za kidini.
Diwani
huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa habari uchapishaji na matangazo kutoka Umoja
wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma,aidha amewataka vijana kujishughulisha
na miradi mbalimbali ili waweze kuondokana na utegemezi katika suala la
maendeleo.
Amesema
baadhi ya vijana walio wengi wahajitumi na muda mwingi wanautumia kwa kukaa
vijiweni huku wakisubiri kufadhiriwa hali ambayo imewasababishia kujikuta
wakutumiwa na shetani kwa kufanya matendo maovu.
Akizungumza
na vijana wa kanisa hilo la Anglikana kwenye uzinduzi huo,amewataka pia
kutumia nafasi zao kuisaidia serikali katika kuhubiri neno la mungu kwa wezao
ambao bado wanaendelea kufanya kutenda vitendo visivyo halali.
“Tumieni
muda wenu kuisaidia serikali katika kuhubiri habari njema za Mungu kwa vijana
wezenu ambao bado wanatumikishwa na shetani na kusababisha kuchukiwa na jamii
inayowazunguka na hata kwa serikali pia”alisema.
Kwa
upande wake Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya dini mkoa wa Dodoma,Dkt Elia Mauza
amewataka vijana kwa upande wao kuhakikisha wanaiombea serikali ya awamu hii ya
tano ili fursa zilizopo ziweze kuwafikia watanzania wote.
Amesema
jukumu la kuiombea Taifa na viongozi waliopo halipo tu kwa madhehebu ya dini na
baadhi ya watu,bali lipo hata kwa vijana ambao wanaoelezwa kuwa ndiyo wenye
nguvu kwa mujibu wa vitabu vitakatifu vya Mungu.
Mwisho.
Post A Comment: