ARUSHA MEYA MSTAAFU WAFIKISHWA KORTINI
Naibu Meya mstaafu
na pia aliyekuwa Diwani wa kata ya Daraja mbili Prospa Msofe na Afisa
mtendaji wake Modesta Lupogo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma tofauti
tofauti zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma
Kesi hiyo ni kesi no 379 iliyoongozwa na Hakimu Mkazi
Mfawidhi Ruwenkiza na wakili wa TAKUKURU Monika Kijazi akishirikiana na Rehema
Mteta ambapo wamesema
Vigogo hao wanakabiliwa na kesi tatu ambapo kesi ya
kwanza ni ya Afisa mtendaji Modesta
Lupogo aliwasilisha nyaraka za uongo za mapato na matumizi kuanzia October hadi
December 2013 ya shilingi million 8 kuwa zilitumika kwenye mradi wa maji katika mtaa wa Alinyanya na
Sanare kata ya Daraja mbili na huku
fedha hizo hazikutumika katika mradi huo bali zilitumika kwa maslahi ya mtu
binafsi
Kesi ya pili inawahusu watuhumiwa wote wawili ambapo walishiriki kutenda kosa
la Ubadhilifu wa fedha za umma ambapo katika sheria ya TAKUKURU ni kosa kifungu 32
Kesi ya tatu inamuhusu Naibu Meya mstaafu na aliyekuwa
diwani wa kata ya Daraja mbili Prospa Msofe kwa kuhusika na Ubadhilifu wa fedha
za umma kuanzia October mosi hadi November 30 ambapo ni kosa katika sheria ya
TAKUKURU kifungu 28(1)kuwa million
8 hazikutumika kwa matumizi
yaliyokusudiwa na halmashauri
Washtakiwa wote wamekidhi masharti ya dhamana ambapo
walitakiwa kuwa na wadhamini wawili wawili watakaosaini bondi ya shilingi
million mbili ,kitambulisho cha kazi kinachotambulika na uchunguzi
umeshakamilika hivyo hoja za awali zitasomwa
October 11
Back To Top
Post A Comment: