MKUU wa Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma  Palolet Mgema  (mwenye tracksuit  ya bluu Pichani )amewaagiza watendaji wote kuanzia ngazi ya Mtaa,Kata na Halmashauri kuanza kuwatoza faini ya sh. 50,000 wananchi wote wasiojitokeza kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi .Ametoa Agizo hilo leo wakati anashiriki usafi kwenye Mtaa wa Miembeni Kata ya Bomba mbili  ambako shughuli ya usafi wa mazingira kiwilaya ilifanyika  katika  mtaa huo,mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Songea.Amemwagiza Afisa Afya wa Manispaa ya Songea Maxensius Mahundi,siku ya Jumatatu Asubuhi kwenda ofisi kwake na majina ya watu 10 ambao wametozwa faini  katika Mtaa wa Miembeni ambako imebainika  wanaojitokeza kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho  wa mwezi  asilimia zaidi ya 90 ni wanawake pekee. Wilaya ya Songea  ina Halmashauri  tatu ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Songea,  Halmashauri ya Wilaya ya Songea  na Halmashauri  ya Madaba

Share To:

msumbanews

Post A Comment: