Home
KIMATAIFA
Ulevi wawaponza abiria 6 wapigwa marufuku kupanda ndege
Ulevi wawaponza abiria 6 wapigwa marufuku kupanda ndege
Shirika moja la ndege limewapiga
marufuku watu sita kuabiri ndege yao wakisema walikuwa walevi wenye
kiburi ,wajeuri, na kubishana ovyo na wahudumu wa ndani ya ndege hiyo.
Shirika hilo liitwao Jet2 limesema vitendo vya kundi hilo la walevi
sita walibughudhi safari ya ndege iliyokuwa inatoka miji ya Uingereza
Newcastle kwenda Tenerife .
Zaidi ya hayo shirika hilo liliwapiga marufuku watatu wa hao kwa
mwaka mmoja, lakini likakataa katakata kuwapa huduma ya usafiri wengine
watatu waliokuwa wanataka kuondoka kutoka kisiwa kimoja cha watalii ili
kurudi makwao.
Msemaji wa shirika hilo la ndege amesema watu hao walikuwa wamelewa chakari hata kabla ya kuabiri ndege hiyo.
Msemaji huyo amenukuliwa kusema; “Watu hao walikuwa
walevi wajeuri na kutaka kuanzisha ugomvi na wahudumu wetu wa ndani ya
ndege . Ni sharti waelewe kuwa matendo kama hayo ya hasa kuwabughudhi
wateja wetu wengine hayawezi kamwe kukubalika na sharti wajue madhila ya
kufanya ushari kama huo.
“Tungependa wateja wetu wafurahi kwa kusafiri kwa amani
na utulivu bila kubughudhiwa na watu wachache wasumbufu, nasi tutafanya
kila juhudi kuhakikisha tabia hiyo inakoma.”
Back To Top
Post A Comment: