Home
MICHEZO
TFF YATANGAZA VIINGILIO VYA MCHEZO WA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza viingilio vya
mchezo wa ‘Watani wa Jadi’ Simba na Yanga wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Jumamosi Octoba mosi.
Simba inakutana na watani wao wakiwa vinara wa ligi baada ya kushinda
Michezo mitano na kutoka sare mmoja huku Yanga wakishinda minne, kutoka
sare mmoja na kupoteza mmoja.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amevitaja viingilio hivyo kuwa VIP A
ni sh 30,000 VIP B & C sh 20,000 na mzunguko utakuwa sh 7,000.
Mashabiki watakaotaka kushuhudia mtanange huo uwanjani watatakiwa
kutumia tiketi za Kielectoniki ambazo ndiyo pekee zitakazowezesha
kuutazama mchezo huo ambao unaziba mianya yote ya kuingia bila kulipa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Selecom ambao ndiyo
wasimamizi wa tiketi hizo Galus Runyeta alisema tiketi hizo zitaanza
kuuzwa kuanzia kesho katika vituo mbali mbali jijini hapa.
Baadhi ya vituo hivyo ni Vituo vya mafuta vya Total, Village
Supermarket, Vituo vya mafuta ya Puma, Samaki Samaki, Buguruni Sheli,
Mlimani City, Sinza Africa Sana na Uwanja wa Taifa.
Aidha Galus amewataka mashabiki wa timu hizo kununua tiketi mapema
kuanzia kesho katika vituo tajwa ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza
siku ya mtanange huo.
Back To Top
Post A Comment: