Madereva wa malori kutoka nchini Tanzania (Pichani na nguo nyekundu) waliokuwa wametekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuokolewa, watawasili nchini leo.Madereva hao juzi walikutana na Gavana wa Bukavu kuzungumza naye kuhusu maswahibu yaliyowakumba katika tukio hilo la kutekwa lililoripotiwa kutokea Septemba 14, mwaka huu nchini humo kabla ya kuokolewa na majeshi ya Congo (DRC).Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyotokewa jana, ilisema madereva hao watawasili nchini leo saa tisa alasiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: