Kwa wale wapenzi wa brudani hii sio ya kukosa kabisa kwani haijawahi kutokea,msanii maarufu wa miondoko ya mtindo wa muziki wa swahili jazz kutoka nchini kenya maarufu kama Juma Tutu atatumbuiza katika jukwaa la Le Patio Hotel Jijini Arusha Ijumaa ya wiki hii.

 Juma tutu anatamba vibao kadhaa ambavyo ameshatoa kama vile Nakupenda kama sukari,undungu na Tahadhari lakini kibao chake ambacho kimempatia umaarufu ni "NAKUPENDA KAMA SUKARI" ambacho kinafanya vizuri katika soko la muziki wa swahili jazz.


 Kwa wal wasiojua aina hii ya muziki hii ni aina fulani ya muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa kiasilia wa Afrika mashariki,Afrika ya kati na bara la Asia.Mchanganyiko wa muziki huu hutupatia radha ya muziki mzuri unaoitwa swahili jazz. 


 Kwa wale wakazi wa maeneo ya ARUSHA na mikoa ya jirani fika Le Patio Hotel siku ya ijumaa ya 30 sept kwa ajili ya kupata burudani ya uhakika kutoka kwa mwanamuziki huyu kutoka 
nchini kenya kwa kiingilio cha shilingi 10000/= tu za kitanzania. 

Tazama video hapo akitumbuiza katika moja ya show zake.

  
Share To:

msumbanews

Post A Comment: