Unajua kwanini Ndege mpya hufanyiwa Sherehe ya Kunyunyizia maji ndege (Water Arch Salute”)

 

Sherehe ya Kunyunyizia maji ndege ni utamaduni uliozoeleka katika tasnia ya usafiri wa anga kote duniani. Utamaduni huu unajulikana kama ‘Water Arch Salute’ hufanyika kwa magari ya zimamoto kujipanga pande zote mbili na kuiweka ndege katikati, hivyo maji hunyunyizwa juu tokea kila pande ya ndege kutengeneza umbo la mviringo kwa juu ‘Arch’. Sehemu nyingine magari mengi zaidi hupangwa na ndege hujunyiziwa maji huku ikitembea katikati ya magari hayo, na chini ya maji hayo yanayonyunyizwa kwa juu.

Zoezi hili la heshima hufanyika ;
i) Pindi kampuni mpya ya ndege inapoanza shgughuli zake ktk uwanja flani wa ndege(Kuzinduliwa kwa shirika jipya la ndege.
ii) Pindi ndege mpya inapokuwa imefanya Safari yake ya kwanza kwa mafanikio, au pindi shirika la ndege linapozindua safari/route mpya ya safari ya ndege zao na kufanikiwa kufika salama.
iii) Pindi marubani, zimamoto na wafanyakazi wengine ktk sekta ya ndege wanapostaafu au kufariki kazini, kuna wakati hupewa heshima ya ‘Water Arch Salute’ kama ishara ya kuutambua mchango wao ktk tasnia hiyo.
iv) Safari ya mwisho kabisa ya mapato ya Ndege flani (Last Revenue Flight ‘katika uwanja husika, au ktk kampuni husika ktk viwanja flani vya ndege.
v) Matukio maalumu au kuazimisha marukio ya kihistoria (anniversary or special occasions)

Hakuna taarifa kamili za uhakika kuhusu wapi au kwanini utamaduni huu wa maji kuanza. Ila utaamaduni huu unakisiwa kuanza miaka ya 1990s, pale ambapo Kiwanja cha ndege cha Salt Like City International Airport/USA ilipoanza kuwapa heshima ya kustaafu Marubani wa kampuni Kubwa ya Ndege ya Delta Air Lines ya nchini Marekani.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: