Home
Kitaifa
SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WAKAZI WA NJOMBE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force iliyotokea jana Sept 19, 2016 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Lilombwi, kata ya Kifanya mkoani Njombe.
Ambapo watu 12 wamepoteza maisha na
wengine 28 kujeruhiwa, basi hilo limepinduka katika kona ya barabara
wakati likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma.
‘Ndugu Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dkt. Rehema Nchimbi naomba unifikishie pole nyingi kwa wote waliopatwa
na msiba, wamepoteza wapendwa wao, wamepoteza watu waliowategemea’
‘Sote tuwaombee wote waliofikwa
na msiba wawe na moyo wa subira, uvumilivu na pia tuwaombee Marehemu
wote wapumzishwa mahali pema peponi Amina’
Back To Top
Post A Comment: