Rais wa Shelisheli James Michel ametangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake. Uamuzi huo ambao ameutoa kupitia hotuba iliyorushwa kwenye runinga mbalimbali nchini humo utatekelezwa tarehe 16 Oktoba mwaka huu.

Tangazo hili amelitoa kufuatia kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa Wabunge, ushindi ambao ulinyakuliwa na upinzani, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kurudi kwa vyama vingi vya siasa nchini Shelisheli mwaka 1993.

James Michel, mwenye umri wa miaka 72, madarakani tangu mwaka 2004, atarejelewa kwenye wadhifa wake na Makamu wa rais Danny Faure.

Chama kimoja cha zamani madarakani tangu mwaka 1977, kilishinda viti 10 vya Wabunge, dhidi ya 15 vya muungano wa upinzani wa Linyon Demokratik Seselwa ("Seychelles Democratic Union").

Madarakani tangu mwaka 2004

Bw Michel, madarakani tangu mwaka 2004, alichaguliwa kwa muhula wa tatu kwa 50.15% ya kura, sawa na kura 193 zaidi ya kiongozi wa upinzani Wavel Ramkalawan.

James Michel alikua rais wa nchi ya Shelisheli mwaka 2004, akimrithi kulingana na Katiba France-Albert RenΓ©, ambapo alikuwa Makamu wa rais. Michel anajiuzulu kabla ya kumalizika muda wake

Posted by ISSACK MBOTERA 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: