Home
BURUDANI
Prof. Ndalichako aitaka Bodi mpya ya TCU kushughulikia matatizo Vyuo Vikuu
Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Bodi
mpya ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) aliyoizindua leo jijini Dar es
Salaam, kushughulikia kikamilifu changamoto zilizoko katika Tume hiyo.
Prof.
Ndalichako ameiambia bodi hiyo kuwa amekuwa akipokea malalamiko kutoka
kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma, hivyo ni
wakati wa bodi hiyo kufuatilia kwa ukaribu malalamiko hayo na kuyafanyia
kazi.
“Tunaelewa
kwamba wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, lakini yapo
malalamiko ambayo yana tija na ni lazima yatatuliwe, kwa mfano
malalamiko yanayohusu uvurugaji wa matokeo au taratibu zinazokuwa
kandamizi kwa wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu,” alifafanua Prof.
Ndalichako.
Akitolea
mfano wa taratibu kandamizi katika vyuo hivyo, Prof. Ndalichako amesema
kwamba mwanafunzi anapopoteza kitabu cha chuo hulipishwa mara tatu ya
gharama ya kitabu hicho huku mwanafunzi huyo akiwa ni mtoto wa masikini
hali inayopelekea wanafunzi kutoazima vitabu wakihofia kulipishwa
gharama kubwa pindi vitabu hivyo vitakapopotea.
Vile vile
amesema kuwa kuna baadhi ya vyuo vimekuwa vikiwataka walimu kutoa
taarifa ya kuacha kazi miezi mitano kabla ya kuacha kazi ambapo sheria
mama inamtaka mwajiriwa kutoa taarifa ya kuacha kazi kwa mwajiri miezi
mitatu kabla ya kuacha kazi.
Aliendelea
kwa kusema kuwa taratibu hizo zinawakandamiza walimu kwani chuo
kinapoamua kumfukuza kazi mwalimu humfukuza papo kwa hapo bila kumpa
muda wa kujiandaa.
Pia
amesema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha
Ifakara mwezi Mei mwaka huu kuhusiana na walimu wa chuo hicho kuvuruga
matokeo yao, lakini chuo hicho akijatoa maamuzi juu ya walimu hao mpaka
hii leo, hivyo kuwaacha wanafunzi kuendelea kubaki nyumbani bila kujua
hatima yao.
Aliongeza
kwamba TCU inamamlaka yote yakuvifuatilia vyuo vikuu vyote nchini
pamoja na kuangalia utendaji kazi wa vyuo hivyo ikiwa unaendana na
viwango vilivyowekwa.
Aidha,
ameitaka TCU kufanya utafiti wa wanafunzi walioko vyuoni ili kubaini
wanafunzi wasio na sifa kutokana na baadhi ya vyuo kuingiza wanafunzi
kinyemela bila kupitia TCU au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE).
Vile
vile, Prof Ndalichako ameitaka Bodi hiyo kutunga sheria ya Vyuo Vikuu
itakayoipa meno tume hiyo kusimamia vyuo vikuu bila kuwa na pingamizi
lolote.
Bodi hiyo
itafanyakazi kwa kipindi cha miaka 3, kuanzia Septemba 28 mwaka huu
hadi Septemba 2019, ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Philip Jacob Mtabaji
Back To Top
Post A Comment: