Pacha walioungana nchini Syria ambao walihamishwa katikati ya machafuko wiki mbili zilizopita wamefariki dunia,mapacha hao walikuwa wanasubiri kibali kutoka nchini humo ili kusafirishwa nje ya nchi ya Syria kwa matibabu maalumu.
Watoto hao pacha wa kiume waliokuwa na umri wa mwaka mmoja, Moaz na Nawras, waliokolewa kutoka katika machafuko walipokuwa wamezingirwa na waasi ambao wanashikilia upande wa eneo la Mashariki ya mji wa Ghouta nje kidogo ya Damascus na kuokolewa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu.
Baada ya kuokolewa, walikimbizwa katika hospitali maalumu ya watoto katika mji wa Damascus. Pacha hao waliokuwa wameungana kuanzia sehemu ya kifuani, walikuwa wanahitaji upasuaji wa dharura nje ya nchi ya Syria.
Wanaharakati wa kambi ya upinzani nchini humo wameishutumu serikali ya Syria , kwa kusema kuwa serikali hiyo imeshindwa kutoa nyaraka muhimu za kusafiria kwa wakati na hivyo kusababisha vifo hivyo.
Post A Comment: