Home
Kitaifa
Mvua ya Barafu Sumbawanga Yasababisha Maafa
Mvua kubwa ya upepo iliyoambatana na mawe ya barafu iliyonyesha jana
jioni katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imesababisha maafa ya
kuanguka nyumba 21, vifo vya mifugo na watoto watatu kunusuirka vifo.
Mwandishi
wetu ameshuhudia wakazi wa kijiji cha Mtimbwa katika Manispaa ya
Sumbawanga wakijaribu kuokoteza mabaki ya bati zilizoezuliwa katika
tukio hilo la mvua ya takribani dakika arobaini na tano na kuzungumza na
baadhi ya wahanga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtimbwa, Wilbroad
andrea Kapufi ameeleza tathmini ya awali imebaini kuathirika kwa nyumba
21 na kaya zaidi ya 50 zikikosa makazi.
Back To Top
Post A Comment: