Naibu
Waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema umefika wakati wa
bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia upya sera ya ukopeshaji ili
waweze kutoka mikopo kwa ngazi ya Astashada kwa masomo ya Sayansi ili
kupata wataalam wengi wa fani hiyo
Mhe.
Mpina amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kwenda sambamba ma mapinduzi
ya maendeleo ya uchumi wa viwanda jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na
wataalam wengi wa mambo ya Sayansi na kuongeza tija katika ustawi wa
maendeleo ya viwanda.
Akiongea
na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo ya elimu ya Visiwani Zanzibar,
amesema Tanzania sasa inataka kuingia katika uchumi wa viwanda jambo
ambalo linahitaji wataalam wengi wa masomo ya Sayansi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Abdul-Razaq Bandru,
amesema kuwa bodi hiyo inafanya marekebisho mbalimbali ikiwemo
kufanikisha mabadiliko ya kanzidata ili kuwafikia wadaiwa kwa urahisi
zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Luhaga ametoa pongezi kwa tume ya taifa ya
nguvu za atomic visiwani Zanzibar na kuwambia kuwa serikali ya Tanzania
itaendelea kuimarisha na kuisimamia ofisi za tume hiyo visiwani
Zanzibar.
Post A Comment: