Balozi wa Malawi afurahishwa na jitihada za Mkuu wa mkoa kuimarisha uhusiano wa nchi mbili 
Malawi yaomba ushirikiano katika biashara, kilimo, utalii na Elimu

– Mkuu mkoa asema kupitia Mkoa wa Mbeya  serikali inajenga meli Tatu  aomba meli hizo zifike  mpaka malawi

– kukamilika kwa meli , uwanja wa ndege kutarahisisha biashara, utalii na usafiri

MKUU WA MKOA WA MBEYA Amos Makalla leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Malawi nchini Tanzania Hon Hawa Ndilowe mkoani Mbeya kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kukuza uhusiano wa nchi mbili 

Kwa upande wa Balozi wa malawi amesifu jitihada za Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa kufanya mikutano YA hadhara mpaka wa kasumulu unaotenganisha Malawi na Tanzania na kupitia kauli zake za kuhubiri amani na ushirikiano zimemfanya balozi kuja Mbeya 

Ameomba ushirikiano zaidi na amehaidi kushirikiana na Tanzania ktk sekta YA kilimo, biashara , utalii na Elimu

Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya  amemwakikishia Balozi wa Malawi ushirikiano na anaomba kuwepo kwa ziara na vikao vya kubadilishana uzoefu na fursa mbalimbali zilizopo ktk nchi mbili 

Amesema Tanzania kupitia Bandari YA Itungi inajenga Meli mbili za mizigo  na meli moja YA abiria zitakazokamilka mwaka huu na hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria na kumuomba Balozi awajulishe watu wa malawi juu YA fursa hiyo na kuitumia

Aidha kukamilika kwa uwanja wa ndege wa songwe pia ni fursa YA kukuza utalii katika mhifadhi za Kitulo na Ruaha

Posted by Lidia Kishia.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: