Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,
Mapema leo amezindua Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaj kwa Mkoa wa
Dar es Salaam.
Uzinduzi huo Umeambatana na Mpango wa Muonekano Mpya wa
Madereva kwa kuwa na Kofia Nguvu 'Helment' za kisasa na Vizibao ambapo
awali wengi wao walikuwa hawanazo kutokana na kutomudu gharama za
manunuzi.
Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwaomba Madereva kuwa
Mabalozi kwa wenzao wanaovunja sheria za Barabarani kwa kupakiza abiria
zaidi ya mmoja 'Mshikaki'. amewaomba Bodaboda kuacha kutumia Vilevi wakati wanafanya kazi zao za
Usafirishaji. "Tumeongeza vituo vya Bodaboda na Bajaj kushirikiana na
SUMATRA ili kurahisisha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam"
Back To Top
Post A Comment: