Meya
wa Kinondoni, Boniface Jacob leo amekabidhi ramsi ofisi baada ya juzi
madiwani wa baraza hilo kugawanywa kwenda katika Manispaa ya mpya ya
Ubungo na wengine kubaki Kinondoni.
Hatua
hiyo, Manispaa ya Kinondoni inafuatia uamuzi wa Serikali kuzigawa
Kinondoni na Temeke ambazo zimezaa wilaya za Ubungo na Kigamboni.
Baada
ya kukabidhi ofisi hiyo Jacob aliwashukuru watumishi, madiwani na
waandishi wa habari kwa ushirikiano walioinyesha katika kipindi cha
miezi saba akiwa kiongozi.
“Narudi
Ubungo home sweet home (nyumbani ni nyumbani), nasubiri ridhaa ya chama
nikipitishwa, nitagombea tena nafasi hii,”anasema Jacob.
Back To Top
Post A Comment: