Aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu,
ameshindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Abdallah Mtolea(CUF) aliyetangazwa
mshindi katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.
Mtemvu aliyekuwa
akitetea kiti hicho katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alifungua kesi
katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipinga matokeo yaliyompa
ushindi Mtolea.
Pamoja na mambo mengine akidai kuwa kura za baadhi ya vituo vya kupigia kura hazikujumlishwa katika matokeo ya jumla.
Hata
hivyo Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa leo na Jaji Issa
Maige aliyekuwa akisiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya Mtemvu na
badala yake imemthibitisha Mtolea kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.
Katika
hukumu hiyo Jaji Maige amesema kuwa Mtemvu ameshindwa kuthibitisha
madai yake jinsi yalivyoathiri ushindi wa mbunge huyo, huku akisema
kwamba kasoro alizokuwa akizilalamikia Mtemvu hakuathiri ushindi wa
mbunge huyo.
Back To Top
Post A Comment: