MBUNGE wa Songea Mjini  Mkoa wa Ruvuma Leonidas Gama

 MBUNGE wa Songea Mjini  Mkoa wa Ruvuma Leonidas Gama  ameamua kuhamishia ofisi yake katika ofisi za kata 21 zilizopo katika Manispaa ya Songea ili kusikiliza kero mbalimbali  zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.Taarifa ya Katibu wa Mbunge huyo imebainisha kuwa  Mbunge amebaini kuwa kuna wananchi wengi wanaishi nje ya Mji wa Songea ambao wanatamani kuonana na Mbunge lakini wanashindwa kutokana na changamoto mbalimbali.Kwa hiyo ili  kuwarahisishia ameamua kwenda kusikiliza kero zao katika  maeneo yao.Ratiba ya awali ya mbunge huyo inaonesha kuwa Jumatatu Septemba 26 na 27,Gama ataweka ofisi yake katika Kata ya Tanga  ambapo  atasikiliza kero za wananchi wa Kata hiyo kwa siku mbili kuanzia asubuhi hadi jioni.Septemba 28 hadi 29 Gama ataweka ofisi yake katika Kata ya Subira.Mbunge huyo pia atamalizia ziara ya kutembelea kata 10 ambazo aliweka kiporo baada ya kwenda kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano Dodoma.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: