Fuvu na vifaa vingine vya mhanga wa Mauaji ya Kimbari katika eneo la kumbukumbu la mjini Kigali, nchini Rwanda.

Serikali ya Marekani imechukua uamuzi wa kumrejesha nyumbani Leopold Munyakazi, mmoja wa wasomi wa Rwanda anayetuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Bw Munyakazi anatuhumiwa kuwa alivaa majani ya mgomba mmoja wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa lengo la kujitambulisha kuwa ni kutoka jamii ya watu wa kabila la Wahutu. Bw Munyakazi pia anatuhumiwa kupanga mashambulizi ya usiku katika nyumba za familia za watu kutoka jamii ya Watutsi.
Awali Leopold Munyakazi alipoteza kesi ya kupata uhifadhi nchini Marekani.

Hata hivyo Leopold Munyakazi, ambaye wakati fulani alihudumu kama muhadhiri wa chuo kikuu nchini Rwanda amekana madai hayo.

Itakumbuka kwamba watu 800,000 kutoka jamii ya Watusti na nWahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika kipindi kisichozidi siku 100, baada ya ndege aliyokua ikimsafirisha rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana kudunguliwa wakati ilipokua ikitua kwenye uwanja wa Kanombe usiku wa tarehe 6 mwezi Aprili mwaka 1994.

Wakati huo Rais Habyarimana alipoteza maisha akiwa pamoja na mwezake wa Burundi Cyprien Ntaryamira. Katika jali hiyo mawaziri wawili wa Burundi katika utawala wa Ntaryamira waliangamia.

Mpaka sasa ni vigumu kujua waliohusika na kuingusha ndege iliyokua ikimsafirisha Aliyekuwa rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: