Home
Unlabelled
MAGARI YA MWENDO KASI DODOMA.
MAGARI YA MWENDO KASI DODOMA.
Baada ya kuanza kwa mafanikio kutoa
huduma za usafiri katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mabasi ya
mwendokasi sasa yanatakiwa yatue mjini Dodoma.
Mbunge wa Kilolo mkoani Iringa, Venance
Mwamoto ameishauri Serikali kuweka mpango wa kujenga njia za mabasi
hayo ili kuepuka msongamano unaoweza kutokea baada ya Serikali kuhamia.
Mwamoto amesema tangu Serikali itangaze kuhamia Dodoma kumekuwa na ongezeko la watu wanaohitaji maandalizi ya huduma mbalimbali.
“Serikali isisubiri Dodoma iwe kama Dar
es Salaam ili tuanze kuhangaika, mabasi ya mwendokasi yatasaidia ujenzi
wa uchumi kwa kasi kwa sababu watu hawatatumia muda mrefu barabarani
kama ilivyo kwa Dar es Salaam, hasa maeneo yasiyo na usafiri huo,”
amesisitiza.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (LAAC)
walipotembelea mradi huo hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Dart,
Ronald Rwakatare alisema hivi sasa wapo kwenye mkakati wa kuendelea na
ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili jijini Dar es Salaam.
Back To Top
Post A Comment: