Maafisa watatu wa serikali na meneja ws CRDB tawi la Bukoba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Bukoba wakituhumiwa kula nja kwa kufungua account ya bandia inayofanana na ile inayotumika kukusanya fedha za waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.


Aliyekuwa Ofisa tawala Mkoa wa Kagera(RAS) Bw Amantius Msole,Aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba BW Kelvin Makonda,AliyekuwaMhasibu wa Mkoa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja CRDB Kagera Karlo Sendwa wamefikishwa mahakamani leo mchana kwa kutengeneza account bandia iliyo na jina sawa na lilioandaliwa na serikali kukusanya fedha kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko mkoani Kagera.


 Wakati ya serikali ikiitwa KAMATI MAAFA KAGERA ikiwa na kianzio cha 0152..wao wamefungua ya jina hilo hilo lakini ikiwa na kianzio cha 0150…Kwa hiyo ya Serikali iliyopitishwa ni 0152225617300 CRDB Bukoba Huku bandia ina jina hilo hilo lakini ikiwa na tofauti ya namba moja tu yahani 0150225617300.
Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamenyimwa dhamana hadi septemba 30,2016 itakapotajwa tena.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: