Leo
September 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya
Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.
Pamoja na kutengua uteuzi wa Prof. Hasa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo. Aidha uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF imeelezwa utafanywa baadaye.
Post A Comment: