PAMOJA
na serikari na wadau kufanya juhudi za kuelimisha wafugaji wa wanyama
mikoa ya nyanda za juu kusini wafugaji hao wanakosa huduma kutoka kwa
wagani ambao wanadaiwa kufanya kazi kwa kusuasua na kuchelewa kutoa
huduma wanapo hitajika.
Wafugaji
hao wamesema kuwa pamoja na kukosa huduma muhimu za matibabu na ushauri
kwa shughuli zao za ufugaji wanaomba serikali kuongeza wagani katika
vijiji vyao ili kufuga kwa tija kutokana na elimu wanayoipata kila
wakati.
Wafugaji
wanaomba serikali kuwasambazia wagani vijijini kwao wakati wakipatiwa
elimu ya kuzitambua fursa za kujiongezea kipato yanatolewa na shirika la
umoja wa mataifa la biashara UNCTAD,
Wafugaji
40 kutoka mikoa miwili ya Njombe na Mbeya Kwenye halmashauri tano za
Rungwe, Wangingombe, Makambako mji, Njombe mji na halmashauri wilaya,
wanatambua fursa za kibiashara zinazotokana na mazingira wanayo ishi.
Serikali nayo inasema kuwa nifaraja kubwa mfugaji wanapo ongezeka kiuchumi.
Mkufunzi
kutoka UNCTAD amesema wafugaji hapo awali walikuwa hawana uwezo wa
kulitosheleza soko la maziwa ndio maana mafunzo yanatolewa mara kwa
mara.
Post A Comment: