Home
KIMATAIFA
Kambi ya Upinzani waandamana dhidi ya rais Kabila DRC
Waandamanaji wameweka vizuizi na
kuchoma magari katika mji mkuu wa Kinshasa nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo,baada ya maafisa wa polisi kuwazuia kuandamana.
Wanamtaka
rais Joseph Kabila ajiuzulu baada ya kukamilika kwa muhula wake mnamo
mwezi Disemba tarehe 20 kulingana na mwandishi wa BBC Poly Muzalia.
Chombo cha habari cha reuters kiliwanukuu mashahidi wakisema kuwa maafisa wa polisi walifyatua risasi kuwatawanya waandamanaji.
Upinzani
unahofia kwamba bwana Kabila ana mpango wa kuchelewesha uchaguzi wa
urais unaotarajiwa mwezi Novemba ili kusalia madarakani.
Maafisa wa uchaguzi na serikali wanasema kuwa uchaguzi huo
utaahirishwa kutokana na matatizo ya mipango katika taifa hilo la
Afrika ya kati.
Taifa la DRC halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlaka ulio huru tangu uhuru wake zaidi ya miaka 45 iliopita.
Back To Top
Post A Comment: