MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Ally Rashid
maarufu kwa jina la Ally Mwizi kifungo cha miaka 30 jela baada ya
kupatikana na hatia ya kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 25,
makaburini.
Hukumu hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wa Manispaa ya Mpanda
ilitolewa jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya
kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kutia
shaka, ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Jamila
Mziray.
Awali Mwendesha Mashtaka Mziray alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa
huyo alitenda kosa hilo Juni 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku katika
makaburi ya Kashaulili yaliyoko katika Mtaa wa Kotazi, Manispaa ya
Mpanda.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa kabla ya kutenda kosa hilo alimfuata msichana
huyo ambaye alikuwa ameibiwa vitu vyake vya ndani ya nyumba ambapo
alimdanganya kuwa ana uwezo wa kumsaidia kuvipata vitu vyote
alivyoibiwa.
Mziray alidai kuwa baada ya msichana huyo kuahidiwa na mshtakiwa kuwa
vitu vyake alivyoibiwa vitapatikana alimlipa mshtakiwa Sh 30,000 ili
akamwoneshe vitu vyake alivyoibiwa.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimpigia
simu msichana huyo saa 2:00 usiku akimtaka waonane ili akamwonesha vitu
vyake vilivyoibiwa.Mziray alieleza mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa
msichana huyo na wakaongozana hadi kwenye makaburi ya Kashaulili ambako
alidai ndiko vilipo vitu vilivyoibwa lakini ghafla mshtakiwa alimpiga
ngwala msichana huyo na kumlawiti huku akimtishia maisha iwapo akijaribu
kupiga kelele.
“Baada ya kumtendea unyama msichana huyo, mshtakiwa alimwomba dada
huyo waende kwenye nyumba ya kulala wageni inayoitwa Kingi Paris ili
wakaendelee kufanya mapenzi zaidi kwa kile alichodai kuwa nyumba hiyo ya
wageni inafaa zaidi kufanyia tendo la ndoa kuliko juu ya kaburi,
Post A Comment: