IGP ERNEST MAGU KUKABIDHIWA SARPCCO.
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu anatarajia
kukabidhiwa uenyekiti wa shirikisho la wakuu wa majeshi ya polisi
kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mkutano unaotarajiwa kufanyika sept.
16 jijini Arusha.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini hapo
msemaji wa jeshi la polisi kamishna Msaidizi wa polisi Advera Bulimba
alisema Mangu atakabidhiwa uwenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa jeshi la
polisi wa nchi ya Msumbiji ambapo atadumu katika nafasi hiyo kwa
kipindi cha mwaka mmoja.
Bulimba alisema mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa
kamati tendaji za SARPCCO ambazo zitakutana sept. 14 na sept. 15 ili
kuandaa ajenda na mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika
mkutano wa wakuu wa polisi ambao unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan.
" Mambo mbalimbali yakiwemo ya kukabiliana na uhalifu wa
kuvuka mipaka yatajadiliwa pamoja na kuweka mikakati na maazimio ya
kufanya Operesheni za pamoja zinazojumuisha nchi zinazounda shirikisho
hilo" alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na majadiliano mbalimbali pia
mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio mbalimbali
kupitia kamati tendaji za wakurugenzi wa upelelezi kamati tendaji ya
sheria, kamati tendaji ya Mafunzo.
Pia kamati tendaji ya mtandao wa polisi wanawake itajadili suala la michezo baina ya majeshi ya polisi kwa nchi wanachama.
Hata hivyo alisema SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwalengo la
kuimarisha ushirikiano wamajeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa
Afrika katika kukabiliana na uhalifu.
"Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na nchi 15 ambazo
ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius na Demokrasia
ya Kongo (DRC)
Nyingine ni Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Shelisheli
Back To Top
Post A Comment: