MWALIMU KULIPA FAINI YA Sh1.6 MILIONI.
BUKOMBE: Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja ya iliyoko wilayani Bukombe, Daniel
Nying’ati (41), ambaye aliomba rushwa ya Sh130,000, atatumikia kifungo
cha miaka mitatu, na akimaliza alipe faini ya Sh1.6 milioni.
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Gabriel Kurwijila amesema ushahidi
uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha shaka, hivyo Mahakama
inamhukumu mshtakiwa kwenda jela miaka mitatu.
Hakimu Kurwijila
amesema baada ya kumaliza kifungo, mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya
Sh1.6 milioni na kutaka adhabu hiyo iwe fundisho kwake na wengine wenye
tabia kama hiyo.
Kabla ya kusomewa hukumu hiyo, akitumia nafasi
aliyopewa kujitetea ili apunguziwe adhabu, mshtakiwa alisema ana familia
inayomtegemea hivyo hakimu amuhurumie.
Back To Top
Post A Comment: