Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa
hatomchezesha tena Yaya Toure hadi atakapoomba msamaha kwa klabu hiyo na
wachezaji wenzake kutokana na matamshi ya ajenti wake.
Toure mwenye umri wa miaka 33 ameichezea City mara moja msimu huu na aliwachwa nje katika kikosi cha vilabu bingwa Ulaya.
Ajenti
wake Dimitri Seluk amesema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa''
na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda
kinyang'anyiro hicho.
Guardiola:''lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza''.
Raia huyo wa Uhispania pia anataka msamaha kutoka kwa Seluk.
Alisema kuwa ni uamuzi mgumu kumwacha nje Toure katika kikosi cha kombe la Vilabu bingwa Ulaya.
''Iwapo
ana tatizo anafaa kuzungumza wenzake katika klabu ,alisema
Gurdiola,ambaye alikuwa mkufunzi wa Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa
Manchester City 2010.
Back To Top
Post A Comment: