MSAADA wa Shilingi bilioni 6.3 umetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyo haribika baada ya kuathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba mkoani Kagera.

Hayo yabainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu huo.

Profesa Ndalichako amesema kuwa msaada huo umetokana na ziara aliyoifanya tarehe 17 na 18 mkoani Kagera ambapo mwakilishi kutoka DFID nchini alishiriki katika zaiara hiyo na kutembelea shule zilizo haribika kutoka na tetemeko hilo.

“Baada ya bunge kuisha tarehe 17 na 18 nilifanya ziara ya kutembelea shule zilizoharibika kutokana na tetemeko, kwa bahati wadau wetu wa maendeleo DFID waliungana name kutembelea shule za Ihungo na Rugambwa kutokana ziara ile wameamua kutusaidia” Alisema Ndalichako.

Kufuatia ziara hiyo ambapo walijionea uharibifu mkubwa wa majengo ya shule ya Ihungo na nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa, DFID waliguswa na athari walizozikuta na kuamua kusaidia ujenzi wa Shule ya Ihungo na nyumba 10 za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa.

Amesema kuwa msaada huo umelenga kujenga upya shule ya Sekondari ya Ihungo ikiwa ni pamoja na kujenga maabara ya kisasa na kununua samani zilizoharibika.

Mpaka sasa wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapo mkoani Kagera mabapo leo wanakabidhiwa shule hizo na Manispaa ya Bukoba ili waanze ujenzi wake unaotarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini (DFID Tanzania) Vel Gnanendran amesema kuwa Serikali ya Uingereza imeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

“Kwa niaba ya Serikali ya Uingereza tunatoa pole sana kwa Mhe. Rais Magufu na waathirika wote wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kwa ni tukio lisilo pangwa”. Alisema Mkuu huyo.

Vel amesema kuwa lengo kubwa la wao kutoa msaada huo ni kuhakikisha miundombinu ya shule zilizoharibika kujengwa haraka ili wanafunzi waweze kurejea mashuleni katika wakiwa katika hali ya kawaida.

“Tumeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la Kagera, Serikali ya Uingereza kupitia ofisi ya DFID Tanzania imetoa msaada wa pound milioni 2.23 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 6.3 za Kitanzania”. Alisema Vel.

DFID ni idara iliyo chini ya Serikali ya Uingereza ambayo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya maendeleo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania

Share To:

msumbanews

Post A Comment: