Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe John Ernest Palingo
Meneja maradi wa TACEI Isac Mushi
Diwani kata ya Mlowo Sebastian Kilindu akionyesha chamzo pekee cha maji kilichobakia
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe John Ernest Palingo amesimamisha
uchimbwaji wa bwawa la samaki na umwagiliaji Kitongoji cha Migombani
kijiji cha Mbimba Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe kwa kukiuka taratibu za
kisheria.
Palingo ametoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kwenye radio
na wananchi juu ya uharibifu wa mazingira hivyo kufanya ziara ya
kushitukiza eneo hilo na kuamua kusitisha ili kufanya uchunguzi wa
vibali vilivyotolewa na Afisa mazingira Wilaya ya Mbozi Hamisi Nzunda
February 18 mwaka huu kufuatia ombi la kikundi cha ufugaji na
umwagiliaji cha Isinizya baada ya ombi la February 15 mwaka huu la
kuomba uchimbaji wa bwawa.
Palingo amesema kuwa barua ya Mwenyekiti wa
wa kikundi hicho Jackson Mwapua ni batili kwa kuwa haikuwashirikisha
wananchi wala mamlaka ya maji, aidha muda wa kuridhia ombi hilo ni
dhahiri unatia shaka ndani ya siku mbili kupitisha mradi mkubwa kama huo
.
Kwa upande wake msimamizi wa Mradi huo Julius Mbembela amesema
walipata baraka zote kutoka ofisi ya kijiji ingawa hakuweza kuonesha
mukhtasari wa kikao hicho cha maridhiano .
Mwenyekiti wa kitongoji cha
Migombani Monica Ngondya amesema yeye hautambui mradi huo na wananchi
wake hawajawahi kushirikishwa chochote.
Naye Diwani wa Kata ya Mlowo
Sebastian Kilindu amesema yeye kama msimamizi wa maendeleo wa Kata
hajawahi kupata taarifa ya ombi la mradi huo bali alipopata malalamiko
ndipo alitembelea eneo hilo na kushuhudia uharibifu wa miti ya asili na
vyanzo viwili kati ya vitatu ambavyo vitasababisha kukosekana maji
kwenye bwawa la TACRI Mbimba ambalo ndilo husaidia usambazaji wa maji
kwa ajili ya matumizi kwa wakazi wa Vwawa na vitongoji vyake.
Naye
Meneja wa TACRI Isaac Mushi amesema bwawa la TACRI limejengwa mwaka 1946
hivyo kuruhusu bwawa hilo kujengwa kungesababisha kituo hicho cha
utafiti kufungwa kwa ukosefu wa maji. Baada ya kujiridhisha na ziara
hiyo Mkuu wa Wilaya Palingo alitoa agizo la kusimamishwa mradi huo na
kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kukaa na mamlaka
zote ili kulipatia ufumbuzi mgogoro huo na kwamba hatakuwa tayari
kufumbia macho kuona taratibu zikivunjwa na hatasita kumchukulia hatua
za nidhamu endapo atabaini ukiukwaji wa sheria.
Back To Top
Post A Comment: