BOMOA BOMOA KIBAHA:
BOMOA BOMOA KIBAHA KUANZA NOVEMBA 24:
Kibaha. Wakazi wa
Kiluvya, Mailimoja hadi Tamko Kibaha waliojenga ndani ya hifadhi ya
Barabara ya Morogoro, wametakiwa kubomoa majengo yao kabla ya bomoabomoa
kuanza Novemba 24.
Bomoabomoa hiyo itawahusu wakazi ambao
majengo yao yamo ndani ya mita 60 kila upande wa barabara na ambao
tayari nyumba zao zimewekewa alama ya ‘X’ kuwataarifu kuwa wamejenga
sehemu isiyo sahihi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo alisema katika kikao cha Bodi ya Barabara kuwa wananchi watambue
kuwa taarifa walizopewa za kubomolewa nyumba zao ni za kweli na
shughuli hiyo itahusu nyumba zilizo ndani ya mita 60 kila upande na siyo
mita 120 zilizotangazwa awali.Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanroads), Tumaini Sarakikya alisema tangazo la awali lililoeleza kuwa
bomoabomoa hiyo, itakayokumba pia soko, itahusu majengo yaliyo ndani ya
mita 120, halikueleweka vyema, bali ni mita 60 kila upande.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo alisema maandalizi ya
kuwahamisha wafanyabiashara wa Soko la Mailimoja yanaenda vizuri na
wametoa maombi maalumu ili kituo kikuu cha mabasi cha Mailimoja
kiendelee kubaki kwa muda eneo hilo wakati mchakato wa kuanza ujenzi wa
kituo cha kisasa ukiendelea chini ya ufadhili wa Benki ya TIB.
Hata
hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpta Mshama alitumia muda mrefu
kuwakingia kifua wananchi hasa
wafanyabiashara wa soko la Mailimoja
wasiondolewe kwanza kabla Tanroads haijajua italitumia vipi eneo hilo na
kwamba halmashauri haijaweka miundombinu kwenye eneo wanakohamishiwa.
“Mimi bado naona tunawasumbua hawa wananchi wakati hawana tabu ya
kuondoka. Wote waliowekewa ‘X’ wanajua siku yeyote wanatakiwa kuondoka,”
alisema.“Lakini napata tabu kwa nini tunawaondoa hasa wafanyabiashara
wa soko huku hatujawaandalia mazingira mazuri.
Tanroads mmekua mnabomoa maeneo mengi tu lakini hamyaendelezi wakati mwingine huwa mapori, sasa kwa nini msisubiri kwanza?”
Back To Top
Post A Comment: