Mgombea Urais kupitia Chama cha
Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton amerejea kwenye mbio za
kampeni baada ya kuugua homa ya mapafu.
Akiongea na mwandishi wa
habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North Carolina, Bi Clinton
alisema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua
hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango
kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.
Back To Top
Post A Comment: