Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi namba ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helmet) ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (katikati) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (katikati) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).
Mshindi wa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga akitoa maneno ya shukran kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) kwa kupata zawadi hiyo. Ni baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Na ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Mombo, kabla ya kukabidhi  pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (hayupo pichani) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).

Na Yusuph Mussa, Korogwe

BENKI ya NMB imeendelea kutoa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama guta, baada ya mwananchi wa Kijiji cha Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Justin Magali (44) kuibuka mshindi.

Akizungumza leo Aprili 5, 2022 kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombo Tawi la NMB Mombo, Meneja wa  Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper alisema washindi wa fedha taslimu pamoja na pikipiki ya miguu mitatu, ni wateja wote wa benki hiyo ambao wameweka akiba angalau kuanzia sh. 100,000.

"Ndugu Watanzania zawadi tulizoziandaa kwa wateja walioweka akiba  ya walau sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB, waliingia kwenye orodha ya wanaostahili kushinda. Mpaka sasa tayari kupitia kampeni hii, tumeshatoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi mbalimbali. Pia tumepata washindi 50 wa pikipiki za miguu mitatu ya mizigo.

"Na huyu wa leo ni mshindi aliyejishindia pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya Sky Mark. Zawadi tulizotoa mpaka sasa zina thamani ya sh. milioni 300. Kikubwa leo tunatoa zawadi kwa mshindi wa Kampeni yetu ya Bonge la Mpango Awamu ya Pili ambayo tumeindesha kwa miezi mitatu iliyopita" alisema Prosper.

Prosper alisema Oktoba, 2021, walizindus kampeni maalumu yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania. Kampeni hiyo ilikuja kwa Awamu ya Pili baada ya mafanikio ya Awamu ya Kwanza iliyofanyika mpaka Juni, 2021.

"Kila wiki kulikuwa na washindi 10 wa pesa taslimu, na washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu. Kila mwisho wa mwezi kulikuwa na washindi watatu wa pikipiki za miguu mitatu, na droo kubwa ya mwisho  tumepata washindi 14 wa pikipiki hizi za miguu mitatu za mizigo" alisema Prosper.

Naye mshindi wa pikipiki hiyo, Magali, akizungumza na waandishi wa habari, amewataka Watanzania kuweka akiba Benki ya NMB, kwani pamoja na kupata zawadi ya fedha taslimu ama pikipiki ya miguu mitatu kupitia Kampeni ya Bonge la Mpango, pia fedha zao zinakuwa salama.

MWISHO.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: