Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Arusha Goodluck Mollel na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya wilaya (Maromboso) kwa tuhuma za kughushi na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu mali ya mwananchi Samandito Gombo .

 Akisoma shitaka hilo mahakamani hapo Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ,James Kiraryo amesema kuwa ,Mshtakiwa na wenzake walitenda kosa hilo mnamo mwaka 2018 katika eneo la Mlangarini. 


Amesema kuwa mshtakiwa huyo akishirikiana na wenzake kwa pamoja walighushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kuuza viwanja ambavyo sio mali yao vyenye thamani ya 30 milioni. 

Amewataja washtakiwa wengine kuwa ni Peter Redding, Joseph Mwaikasu, na Joseph Makona ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kesi ya jinai nambari 406 ya mwaka 2022. 

Hata hivyo washtakiwa hao kwa pamoja walikana kutenda kosa hilo na kisha hakimu kuwaachia kwa dhamana hadi Aprili 25 mwaka huu.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: