Na,Jusline Marco:Arusha

Bodi ya maji Bonde la Pangani imezindua maadhimisho ya wiki ya maji Duniani kwa upandaji miti katika vyanzo vya maji ili kutunza mazingira na kulivya vyanzo hivyo visiweze kuharibiwa na shughili za kibinadamu.

Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe akizindua wiki hiyo jiji Arusha amesema mito na maji yaliyokuwepo wakati wa uhuru kwa sasa yamepungua kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo ujenzi holela kwenye kingo za mito pamoja na utupaji wa takataka katika mito.

Amesema kuwa jiji la Arusha lipo tayari kushirikiana na bodi hiyo katika kuweka alama kwenya hifadhi za mito iliyopo ndani ya jiji la Arusha kli kuweza kufikia malengo ya kuijenda Arusha ya kijani katika miaka ijayo.


"Kizazi cha sasa kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunajali kikazi kinachokuja kwa miaka ijayo kama ambavyo wawee wetu wa miaka ile walivyoweza kutunza vyanzo hivi na hawakukata miti na tokeo yake ndiyo tunayaona sasa hivyo tusiviharibu vyanzo vya maji."alisema Mstahiki Meya wa jiji la Arusha

"Kwa pamoja tushirikiane kuhakikisha tunajenga vyanzo vyetu vya maji ili mito yetu irudi katika uhasili wake kwasababu tusipofanya hivi mwisho wa siku mitu yetu haitakuwa na maji kutokana na uharibifu ambao unatuletea maangamizi makubwa sana" .Alisisitiza Meya Iranqhe

Pamoja na hayo amewataka wananchi wa Kata ya Sokon 1 ambapo miti ...ndipo ilopopandwa katika mto...kuacha tabia ya kutuma takataka ndani ya mito kwani kwa kiasi kikubwa uchafu huo huchangia kutowesha maji hivyo kipitia siku zilizopangwa na jiji za ufanyaji usafi waitumie siku hiyo katika kusafisha vyanzo vya maji ambapo amemuelekeza diwani wa kata hiyo kuisimamia siku hiyo vizuri.

Vilevile ameiomba Bodi hiyo kutengeneza utaratibu wa kutoa elimu kwa wakazi wanaopakana na mito ili wafahamu umuhimu wa mito na kuzingatia maeneo sahihi ya kutupa takataka zao ambapo pia ameomba ushirikiano wa pamoja katika kutunza vyanzo vya maji kusudi maji hayo yaweze kuendelea kuwa masaada kwa wengi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani Segule Segule katika zoezi hilo amesema lengo la upandaji miti katika maeneo ya hifadhi ya mto Ngarenaro ni ili kurudisha uoto wa asili ambao umepotea kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika mto huo.

Ameeleza kuwa kutokana na ushiriki wa kila mmoja katika zoezi la upandaji miti ni ishara kwamba elimu itawafikia wananchi wa eneo hilo na viunga vyake kwani bonde la Pangani lenyewe haliwezi kufika kila mahali ila kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa mazingira na wananchi katika kuendeleza jitihada za utunzaji mazingira na upandaji miti.

"Wananchi wenzangu tusifanye shughuli ambazo zinaenda kunyume na utunzaji endelevu wa rasilimali za maji ambazo ni ulimaji kandokando ya mito na kusababisha kina cha mto kupungua na kusababisha mafuriko."Amesisitiza Segule Segule Mkurugenzi wa Bodi ya maji Bonde la Pangani.

Ameongeza kuwa sheria za utunzaji wa vyanzo vya maji zipo na zinafanya kazia mbapo tayari watu wanaokiuka sheria hizo wanahukumiwa kulingana na makosa yao ambapo amesema si vyema kufika katika hatua hiyo kwani wanaiamini elimu wanayoitoa kwa jamii huku akiwaomba viongozi ngazi ya Kata kutoa msaada wa elimu ya kuzingatia mita 60 za mito ili kuepuka kuingia katika migogoro na bodi hiyo.

Sambamba na hayo Segule ameeleza mikakati yao kama Bodi katika kuhakikisha vyanzo vya maji na mito inaimarishwa ikiwa ni utoaji wa elimu,kubaini maeneo korofi ya mito na kutoa tope lililopo ndani ya mto.

Naye Meneja wa mazingira na usalama kutoka katika kiwanda cha beer cha Arusha Patience Kazahura amesema kuwa ,kama wadau wa mazingira katika kuadhimisha siku ya maji Duniani ipo haja ya kuongeza uelewa kwa wananchi kujua kwamba maji yaliyo juu ya ardhi ni moja kati ya mtaji wa maji yaliyopo chini.

"Kama Tanzania brewers tunayo miongozo ya kuendesha jitihada za kuendeleza mazingira na tunafuata utaratibu wa UN wa kuwa na maji endelevu na kuongeza jitihada katika kulinda vyanzo hata kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili viweze kuwepo kwa ajili ya vizazi vya sasa hivi na vya baadae."Alisema Kazahura Meneja mazingira na usalama TBL






Meya wa Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe akiotesha  mti kwenye kingo ya Mto Ngarenaro kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji Duniani.



Mkurugenzi wa Bodi ya maji Bonde la Pangani Segule Segule ,akiotesha Mti wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yaliyofanyika kwenye Mto Ngarenaro Halmashauri ya Jiji la Arusha.



Meneja  Mazingira na Usalama kutoka Kampuni ya TBL akieleza lengo la wao kushiriki katika maadhimisho hayo ambapo amesema ipo haja ya kuongeza uelewa kwa wananchi kujua maji yaliyo juu ya ardhi ni moja kati ya mtaji wa maji yaliyopo chini.
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: