Kutoka katikati ni Kaimu Msajili wa Bodi ya maziwa Tanzania Noel Byamungu akifuatiwa na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi , akikabidhiwa boksi la maziwa na Mkurugenzi wa kiwanda cha Galax Food Beverages LTD kama ishara ya kufungua rasmi mradi huo
Kutoka katikati ni Kaimu Msajili wa Bodi ya maziwa Tanzania Noel Byamungu,wamkwanza kulia ni Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji Hargeney Chitukuro akikabidhiwa mtindi kama ishara ya kufungua rasmi mradi huo
Kaimu Msajili wa Bodi ya maziwa nchini Noel Byamungu kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa mashuleni
Kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa mashuleni kikiendelea kayika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha |
Irthan Virjee Mkurugenzi wa kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD wanaozalisha maziwa ya Kilimanjaro, akisaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa mashuleni |
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Longido Charles Mbando akisaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa shuleni
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliono ya utekelezaji wa mpamgo wa unywaji wa maziwa mashulemni kilichofanyika leo katika ukumbi ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha
Mwanasheria kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Edwin E. Bantulaki akitoa ufafanuzi wa juu ya makubaliano kati ya Bodi ya Maziwa Tanzania na kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD kuuza maziwa shuleni
Irthan Virjee Mkurugenzi wa kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD wanaozalisha maziwa ya Kilimanjaro, akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa mashuleni
Picha ya pamoja viongozi wa Bodi ya Maziwa Tanzania,waalimu,Ustawi wa jamii mkoa, Kamati ya wazazi,Kkamati ya chakula na uongozi wa kiwanda cha Galax Food Beverages LTD
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Wizara ya mifugo na Uvuvi kupitia Bodi ya Maziwa Tanzania, imeanza utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa shule za msingi ,ukiwa na malengo kuboresha Afya za wanafunzi pamoja na ufaulu wao wakiwa mashuleni
Akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani Arusha, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Noel Byamungu, alisema kuwa mpango huo kwa Sasa umeanza kwa majaribio kwa kuzihusisha shule 13 za msingi za Serikali (9)na binafsi (4)zenye zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo watatekeleza mpango huo kwa miezi 12
Byamungu alisema kuwa shule zilizochaguliwa kuanza mpango huo wa unywaji maziwa,shuleni hizo zinatoka katika Halmashauri za wilaya za Arusha Jiji (8)Arumeru(2) na Longido 3
''Shule hizo ni Upendo friends,Uhuru ,Longido,Namanga,Nalopa,Kaloleni,Meru,Shalom,Makumbusho,Usa River,Leganga,Tengeru English medium na St.Theresa zote ziko mkoani Arusha na makadirio ya wanafunzi elfu kumi''Alisema .
Nae mgeni rasmi katika kikao hicho Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi, alisema kuwa mipango huo ni fursa kwa wafugaji na wenye viwanda vya maziwa kujiongezea kiapato na kukuza Uchumi wa viwanda Nchini
Lyakurwa alisema kuwa mpango huo umelenga kuwajengea watoto utamaduni wa kunywa maziwa, ili baadae kuwe na kizazi ambacho kutakuwa kinatumia maziwa na bidhaa zake, Kama sehemu ya maisha yao yao ya kila siku na kujenga Afya ya Akili na mwili.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka bodi ya maziwa Tanzania Edwin Bantulaki, alisema kuwa Bodi ya maziwa nchini ndiyo chombo kikuu Cha kudimamia Tasnia ya Maziwa nchini hivyo imeamua kuingia makubaliano na kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD kuuza maziwa shuleni
Alisema kuwa malipo hiyo muuzaji atalipwa na kamati ya shule,atakuwa na jukumu la kupeleka maziwa shuleni pia atalipwa punde atakapokabidhi maziwa au atakapokabidhi maziwa awamu nyingine
"Endapo shule husika itashindwa kulipa maziwa kwa muda uliokubaliwa kwa wamu mbili mfululizo Basi shule husika itahesabika kuwa imevunja makubaliano na itawajibika kulipa gharama zoye ambazo muuzaji atakuwa ameishia kw awakati huo" alisema mwanasheria wa Bodi ya maziwa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule waliopo kwenye mradi huo mwalimu Mwl.Mkuu wa shule ya msingi Longido Charles Efatha Mbando alisema kuwa wameupokea kwa mikono miwili,na kuwashirikisha wazazi kwa kutambua kuwa maziwa ni sehemu ya mlo kamili kwa watoto.
Mbando alisema kuwa kutokana na mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi mashuleni ,wanatarajia kwa mwaka 2021 idadi ya ufaulu kwa wanafunzi itakuwa juu kwani maziwa yanajenga Afya uelewa wa wanafunzi mashuleni .
Aidha mpango huu Mkoani Arusha ulianza tarehe 14 Januari 2021 ,wakati timu ya Bodi ya maziwa iliookutana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Afisa (Mifugo,Afisa Elimu,Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Lishe )na wadau wa Elimu .Wazazi ,wakuu wa shule na kamati ya Chakula ya Shule)
Post A Comment: