Wengi wetu tumemuona au kumfahamu nyoka Anaconda kupitia movie tuu lakini kuna mengi sana usiyoyajua kuhusu nyoka huyu basi twende pamoja mpaka mwisho.
Inawezekana Anaconda ndiyo nyoka maarufu zaidi duniani na ndiyo nyoka wakubwa zaidi duniani na anaaminika ndiyo nyoka wanao ogopwa zaidi.
Inaaminika kuwa miaka milioni 60 iliyopita Anaconda walianza kuishi duniani, Anaconda ndiyo mfalme wa misitu ya Amazoni.
Lakini kama ilivyo jamii ya chatu wengine kutokuwa na sumu basi Anaconda nao hawana sumu.
Anaconda huogopwa kwa nguvu na ukubwa wao lakini si kwa sumu kwani Anaconda hawana sumu kabisa.
Anaconda wapo wa aina tofauti tofauti na hutofautishwa zaidi kwa rangi, walio maarufu zaidi ni Anaconda wa rangi ya kijani
Anaconda ndiyo nyoka mwenye uzito mkubwa zaidi duniani anapokuwa mkubwa huwa na uzito wa kilo 70 na wengine hukua mpaka kufikia kilo 250.
Urefu wa nyoka Anaconda hufikia mpaka futi 30 yaani mara 4 na zaidi ya urefu wa Hasheem Thabeet.
Pamoja na kuwa Anaconda ni nyoka mkubwa mno, Anaconda ana uwezo wa kutembea polepole kiasi kwamba hauwezi kumsikia kirahisi hii humrahisishia kazi wakati wa mawindo.
Anaconda anasifika kuwa nyoka anaye jua kujificha mno anaweza kujificha na usimuone kirahisi hata kidogo
Nyoka Anaconda ana kasi zaidi (spidi) akiwa kwenye maji kuliko nchi kavu kama utakuwa na mkosi wa kukutana na nyoka Anaconda basi ni bora ukimbizane naye mkiwa nchi kavu, spidi ya Anaconda akiwa nchi kavu huwa ni ndogo zaidi ukilinganisha akiwa kwenye maji ambako huwa ana spidi kubwa mno.
Anaconda hupendelea zaidi kula nguruwe pori, wanyama kama jaguar na mara chache sana Anaconda ndiyo hula binadamu na anapokula mlo mmoja Anaconda hukaa mwezi mzima bila kula kitu kingine.
Anaconda anapokuwa kwenye giza huona vizuri tuu bila ya shaka yoyote ile kama vile mbwa na paka walivyo na uwezo mkubwa wa kuona kwenye giza bila ya shida yoyote ile.
Maajabu na tofauti na nyoka wengine Anaconda anapotaga mayai huyameza na kuyahifadhi tumboni, muda wa mayai kuanguliwa ukifika watoto hutoka kwa mama yao kupitia mdomo basi hapa inakuja kauli kuwa Anaconda hujifungua kupitia mdomo.
Pamoja na kutisha kwa Anaconda na maajabu yake yote nyoka Anaconda hana sumu kabisaaa.
Post A Comment: