Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini(Brella) Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria
mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze kujua
namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Afisa kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
MWAMKO wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa
Utawala na Fedha wa Brella Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara
Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo
wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Alisema hatua hiyo ni mzuri kwa
sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari
kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni
hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya
kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni
yatakayojisajili
“Baada ya mfumo wa kutoka kwa
vitambulisho vya Taifa na kutakiwa kutumia namba ya vitambulisho idadi ya
makampuni yanayosajiliwa umeongezeka na kufikia idadi hiyo lakini bado
tutaendelea kukutana na wadau kwa kutoa elimu kuweza kuongeza wigo mpaka “Alisema.
Aidha alisema malengo yao ni
kuhakikisha wanapanua wigo mpaka na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha
kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia
mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo.
‘Usajili kabla ya mfumo ulikuwa ni
mkubwa sana lakini ulikuwa unawagharmi wateja wetu kutokana na kwamba wengi
walikuwa wakiibiwa na vishoka kwa sababu wanasafiri kutoka Tanga kwenda Dar
kutokana na kwamba hapo awali kutokuwa na matawi na hivyo kupelekea kuingia
gharama na kuwapelekea mzigo mkubwa hivyo kwa kuliona hilo tukatambulisha mfumo
huo wa kusajili kupitia online na mwamko kabla ya mfumo na baada ya mfumo
mwamko umekuwa mkubwa sana”Alisema
Awali akizungumza wakati wa mafunzo
hayo kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye
pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo
unavyofanya kazi Suzana Senso alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka
mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya
Magharibi na Kanda ya Kati na sasa wapo
kanda ya Kaskazini.
Alisema kwenye maeneo ambayo tayari
wamepita mwamko umekuwa mkubwa sana
kutokana na wafanyabiashara kueleza namna ya mfumo huo unavyofanya kazi ikiwemo
kukutana na maafisa biashara hivyo kuwa chachu ya ongezeko la usajili na uelewa
umeongezeka sana.
Post A Comment: