ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA MRADI WA LNG LINDI LASHIKA KASI

Serikali
kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza
kutekeleza zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi ambao wanaguswa na mradi
wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi.

Mradi
huo ambao unagusa Mitaa mitatu ya Likong’o, Masasi ya Leo na Mto Mkavu
unachukua eneo lenye ukubwa wa hekta 2,071.7, ambapo Serikali imetoa
kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya kufidia wanachi 693 ambao
wanaguswa na mradi huo.

Eneo ambalo kiwanda cha LNG kinatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Likong’o katika Manispaa ya Lindi

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi
alisema, “mchakato wa kuwafidia waathirika wa mradi wa LNG umechukua
muda mrefu sana na nimekuwa nikijibu maswali mengi sana kutoka kwa
wananchi hao.

Hatimaye Serikali imeidhinisha kiasi cha Shilingi
Bilioni 5.2 kufidia wananchi wanaoguswa na mradi huu muhimu. Napenda
kutumia fursa hii kuishukuru Serikali pamoja na Shirika letu la TPDC
kufikia hatua hii muhimu.”

Wananchi
watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi
wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu
Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa
migogoro ya wananchi katika mradi huo


Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa maelezo ya mradi wa LNG mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake.

Katika
hatua nyingine, Meneja mradi wa LNG kutoka TPDC, Mhandisi Fedister
Agrey aliwahakikishia wananchi na vyombo vya habari kwamba, “mradi upo
na ndiyo maana kikosi kazi kutoka TPDC, Benki ya NMB pamoja na Taasisi
zingine za Serikali wapo hapa.”

“Zoezi hili linatekelezwa katika
hatua mbili, hatua ya kwanza inahusisha utoaji wa elimu ya fidia,
matumizi sahihi ya fedha, sharia na utatuzi wa migogoro kwa waathirika
wote wa mradi.

Na hatua ya pili itahusisha zoezi la ulipaji
fidia kwa wananchi husika” alisisitiza Mhandisi Fedister. Wananchi
watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi
wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu
Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa
migogoro ya wananchi katika mradi huo.

Akiongea kwa niaba ya
wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Masasi ya leo Bwana Saidi Ismail Lihoka
alisema, “Tunaipongeza Serikali na Shirika la TPDC kwa kutimiza ahadi
yao ya kulipa fidia wananchi watakaopisha mradi wa LNG.

Pia,
nitumie fursa hii kuwaasa wananchi wenzangu kwamba, wawe watulivu na
wafuate utaratibu uliopangwa na TPDC katika kufanikisha zoezi hili.”
Mhandisi wa Petroli Kutoka TPDC Ndugu Felix Nanguka akitoa mada ya
masuala ya fidia kwa waathirika wa mradi wa LNG katika Mtaa wa Likong’o,
Manispaa ya Lindi Mnamo Desemba, 2015 Serikali ilitwaa ardhi ya
iliyokuwa shamba la mkonge na kuipatia TPDC hati ya umiliki wa eneo hilo
kwa ajili ya kuendeleza mradi wa LNG.

Aidha, uthamini wa
ardhi ya mradi ulifanyika mwaka 2015 na kufanyiwa marekebisho madogo
mwezi Aprili 2017, ili kufidia eneo la ardhi ambalo lilikuwa
linamilikiwa na wananchi pamoja na maendelezo yaliyofanywa na wananchi
katika eneo ambalo limetwaaliwa na Serikali.

Mradi huu ni mkubwa
na wa aina yake kwa Tanzania, ambao Serikali inajipanga vyema ili
kuhakikisha maslahi mapana yanapatikana kwa Watanzania.

Lengo la
mradi huu ni kuiwezesha Tanzania kuzalisha gesi nyingi iliyogundulika
baharini na kuuza rasilimali hii katika soko la Dunia, pamoja na
kuwezesha upatikanaji wa gesi ya kutosha katika soko la ndani kwa ajili
ya kuzalisha nishati ya umeme na matumizi mbalimbali ya viwandani na
majumbani.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )