ZIARA YA MAKAMU WA RAIS KATIKA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI DAR ES SALAAM

 

Leo tarehe 22 Februari, 2021 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea Banda la Tume ya Madini  katika maonesho yanayoendelea katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji  katika Sekta ya Madini unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

 

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Madini unahusisha wadau wa madini ikiwa ni pamoja na Taasisi za Serikali, Taasisi za Kifedha, kampuni za uchimbaji wa madini, wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini nk. 

 

Kauli mbiu ya Maonesho ni  “Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu.”

 

Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )