Wenye Virusi Vya Corona Tanzania Wafika 24

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza uwepo wa wagonjwa wengine wapya wanne wa maambukizi ya virusi vya corona 

Waziri Ummy ametangaza leo Jumatatu Aprili 06, 2020 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari inayoelezea mwenendo wa hali ya corona nchini

Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao wanne, wawili wanatoka Tanzania Bara na wawili wanatoka Zanzibar

 “Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa kesi mpya nne za maambukizi ya virusi vya corona (COVI-19) zilizopatikana Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya kuwepo kwa jumla ya kesi 24 zilizoripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huu nchini” imesema sehemu ya taarifa hiyo

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )