WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA KUTOKA AFRICAB

Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe
uzindua ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya
shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo
vya jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kupambana na maambukizi ya
Corona. Aliyeambata naye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na
Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akizungumza baada
ya kukata utepe kuashiria  uzinduzi wa ugawaji wa mataki 100 ya kunawia
mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya
Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kupambana na
maambukizi ya Corona. Kulia kwani ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix
Lyaniva na Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akikagua moja ya
tanki la maji kati ya mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya
shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo
vya jijini Dar es Salaam kupambana na maambukizi ya Corona.

 Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha
ya pamoja na  viongozi wa kampuni ya Africab baada ya kuzindua ugawaji
wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50
yalitolewa na kampuni hiyo  kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam
ili kupambana na maambukizi ya Corona.
 
Na Said Mwishehe

KATIKA
kuendelea kukabiliana na virusi vya Corona nchini, SerikaIi kupitia
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imepokea msaada wa matanki 100
kutoka kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme ya AFRICAB maalumu kwa
ajili ya kuwawezesha wanafunzi na wanavyuo jijini Dar es Salaam kunawa
mikono ili kukabiliana na janga la homa mapato inayosababishwa na virusi
vya Corona.

Akipokea na kisha kukabidhi matanki hayo yenye
thamani ya Sh. Milioni 50, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Prof.Joyce Ndalichako mbali na kushukuru kwa msaada huo, amefafanua
kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo vyuo na baadhi ya shule
nchini zimefunguliwa na itawawezesha wanafunzi kujikinga dhidi ya
ugonjwa huo wa Covid-19.

Ameongeza kuwa msaada wa matanki hayo
yenye ujao wa lita 1000 kila moja yametolewa kwa shule 10 za Sekondari
za Serikali na 57 kwa shule za sekondari za binafsi na vyuo 13 ni muhimu
kwa Serikali hasa wakati huu ambapo vita dhidi ya ugonjwa huo
unaendelea.

Profesa Ndalichako amesema kuwa “Naiwapongeze AFRICAB
msaada huu muhimu kwa ajili ya kinda afya za wanafunzi wetu, niwaombe
wadau wengine muige mfano huu kwa ajili ya manufaa ya watu wote wa taifa
hili,”amesema Prof.Ndalichako na kuongeza licha ya hatua mbalimbali
zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika napambana dhidi ya Corona,
wananchi nao wanapaswa kuchukua tahadhari hizo huku wakiendelea kuchapa
kazi.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa AFRICAB David Tarimo,
ametumia nafasi hiyo kueleza msaada umetolewa kwa lengo la kuunga mkono
juhudi za Serikali katika kukabiliana na Corona na kusisitiza kuwa wao
kama wadau wa maendeleo na wawekezaji wazalendo huo ni wajibu wao wa
kimsingi.

“Mapambano dhidi ya Corona ni wajibu wa kila mmoja wetu
na sisi AFRICAB tunatambua nini kinafanywa na Serikali katika
kukabiliana na ugonjwa huo unaoisumbua dunia kwa sasa.Aidha mbali na
msaada huo, AFRICAB itaendelea kushirikiana na Serikali katika masala
mbalimbali ya kimaendeleo huku ikitarajia kujenga cha uzalishaji wa dawa
za binadamu hivi karibuni ” amesema.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa
kiwanda hicho Mohammed Ezz amesema kwamba anatoa shukrani za dhati kwa
Rais John Magufuli kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji
yanayokiwezesha kiwanda hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo.”
Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo ameweka mzingira mazuri ya
uwekezaji na hii imekuwa fursa kwetu kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia
ubora ww viwango vinavyotakiwa.”

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )