WAZIRI MPINA ASHTUKIA UPIGAJI WA BILIONI 2.6 UJENZI MAABARA YA UVUVI, AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA NDANI YA SIKU 7

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata maelezo ya namna ya shughuli ya
ujenzi
wa mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania
(TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam  kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya
Petra Constuction co. Limited, Nicholaus
Mlayi alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga
Picha
Wetu.

 Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata ufafanuzi kutoka kwa Mshauri Mwelekezi
wa Kampuni ya Y&P Architect inayosimamia Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam, Anna Shayo alipotembelea mradi
huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu


Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia ramani ya mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi
ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam baada ya kutembelea
kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo na kuunda tume kuchunguza mradi
huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI, Dk. Ismael Kimerei . Picha na Mpiga
Picha Wetu.

Na
Mwandishi Wetu

WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa
Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya
Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama
halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya
fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo
Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha
wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya
Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

Akizungumza
mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  jijini Dar es Salaam, Waziri
Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo
ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa  wa
sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa
wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha
za umma.

Waziri
Mpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na
Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali
ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hata
hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye
mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina
kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500
jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za
mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya
mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina
akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini
ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya
kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na
hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.


Hivyo Waziri Mpina
akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli
utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini
 kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa
ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha
za umma.

 “Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo
na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ
ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba
iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji
Waziri Mpina

Hivyo
Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo
Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa
ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo
muhimu la utafiti.

“Nitaleta
timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo
hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata
mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya
uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na
kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Meneja
wa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la
Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya
shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra
Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.

Luhanga
alisema mradi huo unajumuisha  pia ujenzi
wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya
mvua na kujenga mnara wa maji.

Mkandarasi
wa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia
asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika
mwezi Aprili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote
aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha
‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa
wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )