WAZIRI MKUU MAJALIWA KUANZA ZIARA MKOANI TANGA KESHO

 MKUU wa Mkua wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa
habari mkoani humo leo  ambao hawapo pichani kuhusu ziara maalumu ya
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa itakayoanza kesho Jumatatu

MKUU wa Mkua wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa
habari mkoani humo kuhusu ziara maalumu ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa itakayoanza kesho Jumatatu mkoani hapa


WAZIRI
mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili jijini Tanga kesho June Mosi
Mwaka huu kwa ziara maalum ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa agizo
lake kwa bodi ya Mkonge alilolitoa mapema mwezi machi mwaka huu.

Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkuu wa mkoa wa Tanga Martin
Shigela alisema waziri mkuu anatarajiwa kuzindua Jengo la Bodi ya Mkonge
lililopo Jijini Tanga na baadae atatembelea Taasisi ya utafiti ya
Mlingano na kukagua vitalu vya zao hilo.

Shigela alisema kuwa
ziara hiyo ni mahususi kwa ajili ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa machi
1, mwaka huu baada ya kupokea taarifa ya kamati maalum aliyounda kwa
ajili ya ufuatiliaji wa mali za bodi ya mkonge.

“Baada ya
taarifa hiyo yapo maelekezo aliyoyatoa, hivyo ziara yake hii ni mahususi
kwa ajili ya kuja kuona maagizo aliyoyatoa ya ufuatiliaji wa kufufua
zao la mkonge na namna ya utekelezaji wa urejeshwaji wa mali ambazo
zilitajwa kuwa zilizoporwa kinyume cha utaratibu na sheria” alifafanua.

Aidha
Shigela aliwashukuru na kuwapongeza waandishi wa habari mkoani humo kwa
namna walivyowajibika na kushirikiana katika nyanja mbalimbali
kufanikisha utoaji wa taarifa kwa wananchi kwa urahisi na wakati.

“Niwashukuru
sana ninyi waandishi wa habari kwa namna mlivyowajibika katika ile
ziara ya waziri mkuu pamoja na kupigania kwa pamoja mapambano dhidi ya
corona na kuwatetea wananchi wetu hasa katika eneo la mpakani kule
horohoro” alieleza.

Hata hivyo Shigela aliwataka waandishi wa
habari kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya siku moja kwani ziara
hiyo inalenga kuleta manufaa kwa mkoa wa Tanga kupitia zao la mkonge
kutokana na kwamba ndio zao kubwa linalotegemewa kibiashara.

Alibainisha
kwamba ujio wa Waziri Mkuu Majaliwa ni ukombozi kwa mkoa wa Tanga kwani
endapo zao la mkonge litafufuliwa na kuimarika mkoani humo wananchi
wataweza kujikwamua kiuchumi kutokana na kilimo cha zao.

“Ziara
hii kwetu sisi ni ukombozi mkubwa kwasababu zao la mkonge kwa mkoa wa
Tanga ndio zao mahususi na ndio zao kuu tunalolitegemea katika mazao ya
biashara, na tuna uhakika tukifufua zao letu la mkonge tutakuwa na
uhakika wa wananchi wa wananchi wetu kujikwamua katika umasikini”
alisema.

Ziara hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa itakuwa na lengo la
kufuatilia utekelezaji wa majengo pamoja na mashamba ya bodi ya mkonge
yaliyokuwa yamechukuliwa na wananchi kinyemela kwa maslahi yao ambapo
baadhi yao kuweka taasisi zao binafsi huku bodi hiyo ikiwa haina ofisi
mkoani humo.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )