Waziri Mkuu: Hospitali Wilaya Kibaha itatumika kulaza wagonjwa wa Corona

Na.WAMJW-Kibaha

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya Kibaha ambayo itatumika kulaza  watakaobainika kuwa na Virusi vya ugonjwa wa Corona (Covid19).

Mhe.Kassim Majaliwa amesema  hospitali hiyo itatumika kulaza watu walioambukizwa ugonjwa huo  na kwamba itatumika kwa muda na baada ya ugonjwa huo kwisha itaanza kutoa huduma nyingine za afya.

Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi wa Wilaya ya Kibaha kuwa watu wenye maambukizi ya VIRUSI vya  COVID 19 watalazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku 14 na baada ya uchunguzi ikibainika hawana ugonjwa huo wataruhusiwa kurejea nyumbani.

Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Corona na amezikumbusha familia kuwa na utaratibu wa kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na sabuni au  kutumia vitakasa mikono (sanitizer).

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimweleza Waziri Mkuu kwamba hospitali hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni394 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali hiyo.
Q

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )