Waziri Jafo Aridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi, Jafo alisema: “angalau sasa naanza kuiona hospitali ya Uhuru, naamini nikija baadaye nitaona sura ya jengo.

“Nimeridhika na kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Uhuru na hatua iliyofikiwa, naamini nikija tena hapo baadaye basi kuna jengo litaonekana haoa.”

 Jafo ameendelea kuuagiza uongozi wa Suma JKT kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa hospitali hiyo ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.
 “Nimefurahi kuwa sasa mko katika maandalizi ya kumwaga zege ya renta, hakikishani maandalizi hayo yanakamilika kwa muda mfupi ili tena muongeze nguvu kazi ili zege limwagwe kwa siku moja au mbili.”

 Katika siku za hivi karibuni, Jafo amekuwa akifanya ziara za kushitukiza katika ujenzi wa hospitali ya Uhuru kuona na kukaguza ujezi wa hospitali hiyo.

 Naye Msimamizi wa mradi wa SUMA JKT, Gerlad Mkwele alisema hatua waliyofikia ni kufunga maboksi tayari ya kumwaga zage ya rinta ili ndani ya wiki mbili tume tumeshakamilisha umwagaji wa zege.
“Kama unavyoona tumeshapandisha kuta, tuchaofanya sasa ni kufunga boksi za jengo nzima ili tumwage zege kwa wakati mmoja, na baada ya wiki mbili tutakuwa tunaaza hatua ya pili ya kujenga katika ghorofa ya kwanza.”

Naye Mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Athumani Masasi alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha inasimamia kwa karibu na kuhakikisha ujenzi wa hositali hiyo unafanyia katika muda ulipangwa.

 Hospitali ya Uhuru inajengwa kwa gharama ya Sh bilioni 3.99, fedha zilizotolewa na Rais Magufuli baada ya kuahirisha Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru, Desemba, 9 mwaka 2018 na zile zilizotokana na gawio la kampuni ya Airtel.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )