WATOTO WA MARAIS WA ZAMANI ZANZIBAR WAENDELEA KUJITOKEZA KUCHUKUA FOMU

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR

Mtoto wa Rais wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  (SMZ), Mussa Aboud Jumbe amekuwa mtia ni wa 30 kuchukua fomu ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM-Zanzibar.

Mussa Aboud Jumbe aliwasili majira ya saa Nane mchana na kwenda kuchukua fomu hiyo kwa Katibu wa Kamati maalum CCM-Zanzibar, Cassian Galos  inayolipiwa Milioni moja.

Hata hivyo Mussa Aboud Jumbe hakuwa tayari kuzungumza na wanahabari ambapo alipanga kuzungumza mara tu atakaporejesha kutokana na muda kuwa mdogo.

Kwa hatua hiyo Mussa anakuwa wa Tatu kati ya Watoto wa Marais wa waliokwisha kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao tayari nao wamechukua fomu na kurejesha.

Watoto hao ni pamoja na Balozi Ali Karume Mtoto wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume  na  Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliyekuwa mtoto wa Rais wa Tatu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mwisho.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )