Watano walazwa, 16 waruhusiwa ajali basi la Coast Line

 


Majeruhi wa ajali ya basi la kampuni ya Coast Line lililokuwa likitoka Arusha kwenda Musoma wamelazwa hospitali ya Nyerere huku 16 wakitibiwa na kuruhusiwa.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo,  Tanu Warioba amesema kati ya waliolazwa mmoja ana hali mbaya na amepewa rufaa kwenda hospitali ya Bugando Mwanza baada ya kubainika kuwa ana tatizo kwenye ubongo.

“Ajali imetokea kati ya saa saba mchana ndani ya Hifadhi ya Taifa na wamefikishwa hapa saa 10 jioni, tumewahudumia 16 wakaruhusiwa wakabaki watano ambao wana majeraha sehemu mbalimbali za mwili, “amesema.

Dk Warioba amawataja majeruhi waliolazwa kuwa ni Tumaini Wambura, Rose Dickson, Denis William, Veronica Wambura na mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Masai ambaye amepewa rufaa kwenye Bugando Mwanza kwa ajili ya matibabu.

Rose Dickson aliyeumia bega na mkono amesema mwendo kasi umesababisha ajali kwa sababu kulikuwa na utelezi,  na kwamba basi lilipinduka na wengi waliumia kwa kuangukiana.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )