WANANCHI WASHAURIWA KULIMA KILIMO CHA MATONE BADALA YA KILIMO CHA MAZOEA KINACHOHARIBU MAZINGIRA


 Meneja wa kanda ya kaskazini NEMC,Lweis Nzali akizungumza na waandishi
wa habari Jana ofini kwake ,akiwataka kutumia vyombo vya habari
kuelimisha wananchi juu ya matumizi ya mbinu mbalimbali za asili na za
teknolojia rafiki za kuhifadhi mazingira Afisa mazingira NEMC, Josephati Antony akizungumza na waandishi wa habari akiwataka wananchi kulinda mazingira.

Sehemu ya waandishi wa habari

 


 Na Pamela Mollel, Arusha.KUELEKEA
kilele Cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika
Juni 5  ya kila mwaka wananchi wameshauriwa kulima kilimo cha matone
badala ya kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikiharibu mmomonyoko wa
ardhi na kusabisha uharibifu wa mazingira


Hayo yameelezwa leo
Juni 4,2020 na Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Lweis Nzali alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba kutumia vyombo vya
habari kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya mbinu mbalimbali za asili
na za teknolojia rafiki za kuhifadhi mazingira


Amesema kuwa siku
ya mazingira kitaifa yalikuwa yafanyike mkoani Lindi lakini kutokana na 
janga la ugonjwa wa Covid-19,imeamuriwa maadhimisho hayo kufanyika kwa
kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ili kuepuka
mikusanyiko ya watu wengi ambayo inaweza kusabisha maambukizi ya virus
hivyo.


Ameongeza kila mkoa utafanya maadhimisho kwa kutumia
vyombo vya habari vilivyopo katika maeneo yao.Aidha amesema Tanzania
inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaotokana na
matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za kimazingira


Amezitaja
changamoto hizo kuwa uharibifu wa ardhi,ufyekaji na uharibifu wa misitu,
uharibifu wa vyanzo vya maji, uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini
na upotevu wa bioanuai


Kwa upande wake Ofisa Mazingira wa NEMC
Josephati Antony amesema kuwa ili kulinda na kuhifadhi ikolojia ya
mito,sheria ya mazingira ya mwaka 2004,sheria ya ardhi Namba 4 1999 ,
sheria ya mipango miji 2007,sheria ya usimamizi wa Rasilimali za maji
2009 zinazuia shughuli za binadamu eneo la hifadhi ya mita 60 ambalo
linapimwa kutoka kingo za mito


Ameongeza kuwa  maeneo ya hifadhi
ya mita 60 kutoka kwenye kingo za mito yana umuhimu mkubwa katika
hifadhi ya maji na utoaji wa huduma ikolojia kwa binadamu yaani hewa
Safi na makazi ya viumbe.Kauli mbiu ya mwaka huu inasema hivi “Tuhifadhi
azingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )